September 8, 2021


 ABDI Hamid Moallin ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Horseed Football Club ambao ni wapinzani wa Azam FC ya Dar es Salaam katika Kombe la Shirikisho.

Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kina kazi ya kusaka ushindi mbele ya timu hiyo kwenye mchezo wa awali.

Katika mchezo wa hatua ya awali unaotarajiwa kuchezwa Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex, mbinu za Lwandamina zitapambana na mbinuza Moallin.

Timu hiyo yenye maskani yake Somalia ilianzishwa mwaka 1971 na ni mabingwa mara 8 wa Ligi Kuu ya Somalia na inatumia Uwanja wa Banadir, uliopo Somalia.

Uwanja huo una uwezo wa kuchukua jumla ya watazamaji 15,000.

Mataji yake ilikuwa ni mwaka :-1972,1973,1974,1977,1978,1979,1980,2020/21.

Azam FC tayari ipo Dar baada ya kuweka kambi nchini Zambia na kwa sasa inajipanga kwa ajili ya mchezo huo ujao ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

2 COMMENTS:

  1. Mchezo huo hautakuwa na ushindani sana sana utakuwa wa upande mmoja tu!

    ReplyDelete
  2. Sure azam hata timu ya taifa ya Somalia lazima awafunge tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic