SIMBA imevimba na usajili mpya wa beki wa kulia, Israel Mwenda ambapo kauli ya Kaimu Msemaji wa Simba Ezekieli Kamwaga, imeanika kwamba tayari usajili wake umeonekana kulipa kwa Didier Gomes, ambapo sasa amelazimika kumweka kando staa wake, Shomari Kapombe, na kutoa fursa kwa kinda huyo.
Msimu uliopita, Gomes alionekana kukosa mbadala sahihi wa Kapombe na kulazimika kila mara kumtumia katika kila mechi, baada ya David Kameta ‘Duchu’, kushindwa kuonyesha upinzani aliokuwa akiuhitaji jambo ambalo sasa limezibwa na kinda huyo kutoka KMC.
Taarifa ya Kaimu Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga imelijuza Championi Jumatatu kwamba ni wazi sasa kocha wao Gomes ameshusha pumzi yake baada ya kufanikiwa kupata mbadala sahihi wa Kapombe, jambo ambalo mwanzo lilikuwa likimnyima usingizi.
“Mashabiki wetu wengi awali walikuwa hawaamini katika usajili wetu wa vijana wenye umri mdogo tuliowapa nafasi msimu huu, ila kiukweli kwa benchi la ufundi sasa hivi linachekelea tu baada ya sajili hizi kuonyesha matunda hasa ukianza na safu ya ulinzi wa kulia, ambapo tumemuongeza Mwenda.
“Mwenda ana kiwango bora sana kiasi kwamba amemshawishi kocha, hadi hawazi tena kuhusu Kapombe hata akiumia kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Kamwaga
Kijana apambane, taifa linamtegemea
ReplyDeleteSimba inazidi kufunguka, kupanuka na kunawiri kinyume alivitegemea yule alieitakia mabaya kwani yameanza kumbabaisha
ReplyDeleteSimba ni Laval nyingine
ReplyDeleteTusubiri, msianze mihemko hapo baadae
ReplyDeleteSafi sana kuwa wachezaji wengi wenyekiwango ususani wazawa
ReplyDeleteTusubili muda utaongea
ReplyDeleteIpo vizuri. Watajijua huko huko. Kuwa na sub ya Kapombe ni nzuri Sana.
ReplyDeleteSub ya shabalala sijaona
ReplyDeleteKtk huu usajiri mpya
Mbona heading na kilichoandikwa Ni tofauti? Kappmbe tunamuombea asiumie ili azidi kuleta ushindani wa namba
ReplyDeletekapombe Ni mkali isipokuwa Ni vema beki namba mbili wakiwa wawili inakuwa fresh zaidi
ReplyDelete