September 2, 2021

 


MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Crescentius Magori amefunguka kuwa hana mashaka na uwezo wa beki mpya wa klabu hiyo, Henock Inonga ambapo amemtabiria makubwa ndani ya kikosi hicho kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.


Baka amejiunga na Simba msimu huu, akitokea DC Motema Pembe, ambapo beki huyo raia wa DR Congo amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha Simba, beki huyo pia anamudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji. Akizungumzia ishu hiyo, Magori alifunguka:

 

“Usajili ambao umefanyika msimu huu kwa kiasi kikubwa umezingatia mahitaji ya benchi la ufundi, wachezaji wengi ambao tumewasajili umri wao ni mdogo hivyo ni faida kubwa kwenye kikosi chetu kwa misimu mingi.



“Miongoni mwa wachezaji ambao tumewasajili ni beki Henock Inonga ambaye tumemtoa DC Motema Pembe, sina shaka juu ya uwezo wake na nina imani atafanya makubwa ndani ya kikosi cha Simba msimu huu.”

 

Kikosi cha Simba tayari kimeshawasili nchini baada ya kuweka kambi ya wiki mbili nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya wa mashindano kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ambayo Simba wataanzia hatua ya pili ya michuano hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic