UONGOZI wa Dodoma Jiji umebainisha kuwa sababu kubwa iliyowafanya wakaweka chimbo Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 ni mazingira ya utulivu pamoja na uwepo wa mashabiki wao.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata ilimaliza ikiwa nafasi ya 8 baada ya kucheza jumla ya mechi 34 ilikusanya pointi 44 kibindoni kwa msimu wa 2020/21.
Kwa msimu wake wa kwanza baada ya kupanda ligi imekuwa na mwendo mzuri na kufanikiwa kumaliza ndani ya 10 bora huku ikiongozwa na kocha ambaye aliipandisha kutoka Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Dodoma Jiji ambayo ina maingizo mapya pia ikiwa ni pamoja na Joram Mgeveke aliyekuwa akicheza ndani ya Mwadui FC, Hassan Nassoro kiungo aliyekuwa akikipiga Polisi Tanzania alisema kuwa Moro kuna mashabiki wao.
“Tupo Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, sababu kubwa ya kuwa hapa mbali na mazingira mazuri ya utulivu pia tuna mashabiki wetu ambao huwa wanakuwa nasi bega kwa bega tunapocheza.
“Kikubwa kwa msimu mpya tupo tayari na tunajua kwamba ushindani utakuwa mkubwa, mashabiki waendelee kuwa nasi hakuna haja ya kuhofia tutafanya vizuri bila mashaka,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment