September 14, 2021


 OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameushauri Uongozi wa Yanga kwa kuutaka ujifunge kibwebwe katika maandalizi ya kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya awali dhidi ya Rivers United.

 

Barbara ametoa ushauri huo, baada ya kupata uzoefu wa kutosha kwenye michuano hiyo msimu uliopita, ambapo Simba ilianzia nchini Nigeria kwa kucheza dhidi ya Plateau United, ambapo iliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na Clatous Chama.

 

Kiongozi huyo amesema Uongozi wa Yanga unapaswa kufuata utaratibu wa kujihami wakati wote wa kuelekea mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya wenyeji wao Rivers United, utakaopigwa Jumapili (Septamba 19), Uwanja wa Yakubu Gowon, mjini Port Harcourt katika jimbo la Rivers.

 

Barbara amesema kuna mambo mengi sana ya kuzingatia pindi mjumbe wa Yanga atakapokua nchini Nigeria, huku akisisitiza mjumbe huyo awe tayari kwa kuona mambo tofauti atakayothibitishiwa na maafisa wa idara zote nchini Nigeria, hivyo asiwaamini kwa asilimia 100.

 

“Wajipange sawa sawa kwa sababu ugenini kuna mambo mengi hasa kipindi hiki cha Covid 19, atakayetangulia kule awe makini sana.

 

“Maafisa wa idara zote wanaweza kukuaminisha kila kitu kipo vizuri, lakini siku maalum ikifika unaona mambo yanageuka ili kukutoweni kwenye mchezo, kama hawatokua imara watapoteza mchezo kwa mara ya pili.” amesema Barbara.

 

Tayari Uongozi wa klabu ya Yanga umeanza maandalizi ya kuelekea mchezo wa mkondo wa pili, wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Rivers United, utakaopigwa Jumapili (Septemba 19) nchini Nigeria.

5 COMMENTS:

  1. Watapigwa tena hao UTOPOLO hamna kitu

    ReplyDelete
  2. Amesema kweli wakizingatia watapambana

    ReplyDelete
  3. Wao walisema kuwa fursa ya kushiriki katika mechu hizo wamezipata kwa juhudi zao na wala sio kutokana na mafanikio ya Simba na matokeo ndio tumeyaona

    ReplyDelete
  4. yanga wenyewe wameitumia covid -19 japo haikuwasaidia, eti.wachezaji muhimu wanne akiwepo kipa namba moja eti ana korona.
    refa kawabeba bado hawabebeki. nenda huko mgongwe mrudi mwendelee na uchawi wenu, mnataka kumwachia nani 😂😂😂😂

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic