MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amesajiliwa kwa mkopo wa msimu mzima na Klabu ya Ubelgiji, Royal Antwerp FC akitokea Klabu ya Uturuki, Fenerbahce.
Mzawa huyo anayepeperusha bendera ya Tanzania sera yake namba moja ni haina kufeli ana kazi kubwa ya kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania.
Samatta amewahi kucheza katika Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa na Klabu ya KRC Genk na kuisaidia kuwa Bingwa miaka miwili iliyopita kisha kuhamia Aston Villa na kisha kwenda Fenerbahçe.
Amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania akiwa ni nahodha ataungana na timu Congo kwa ajili ya mchezo dhidi ya DR Congo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 2.
0 COMMENTS:
Post a Comment