September 1, 2021


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo Septemba Mosi wanatarajia kuzindua uzi mpya kwa ajili ya msimu wa 2021/22.


Ni kazi ya Vunja Bei ambaye ana tenda ya kubuni na kutambulisha uzi mpya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Msimu wa 2020/21 iliweza kuwa na jezi za aina tofauti ikiwa ni pamoja na  iliyokuwa maalumu kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na ilikuwa na nembo ya Visit Tanzania. 


Pia walikuwa na uzi maalumu kwa ajili ya Kombe la Shirikisho ambalo walilitwaa kwa kushinda bao 1-0 mbele ya watani zao wa jadi Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.


Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa leo uzi wa mabingwa utajulikana.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic