NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amebainisha kuwa ujio wa Cedric Kaze ndani ya kikosi hicho utawaongezea jambo la kipekee katika harakati za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kaze alikuwa ndani ya Yanga msimu wa 2020/21 alifutwa kazi kutokana na mabosi wa timu hiyo kueleza kuwa mwendo wa timu hiyo ulikuwa ni mbovu ila amerejeshwa msimu huu wa 2021/22 akiwa ni Kocha Msaidizi.
Nahodha huyo amesema:”Uwepo wa Kaze ndani ya Yanga una jambo nzuri kwa sababu alishawahi kutufundisha na anatambua namna ligi ya Tanzania ilivyo.
“Kwa kuwa hatukuwa na kocha msaidizi na yeye amekuja wakati huu imani yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri na tutapambana ili kupata matokeo chanya.
"Jambo la msingi ni mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega nasi katika kazi ambayo tunafanya tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,".
Mchezo wa ufunguzi wa ligi, Yanga ilicheza dhidi ya Kagera Sugar na iliibuka na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba ilikuwa ni Septemba 29.
Bravo
ReplyDelete