September 2, 2021


 NYOTA Cristiano Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno kwa sasa ni mali ya Manchester United, mabao yake mawili ya dakika za lala salama katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia yamemfanya avunje rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwenye timu za taifa.


Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani, dakika 90 ubao wa Uwanja wa Algarve ulisoma Ureno 2-1 Republic Of Ireland ambapo ni wao walianza kupachika bao mapema kabisa dakika ya 45 kupitia kwa John Egan dakika ya 45 na ngoma ilisawazishwa na Ronaldo dk 89 na kumfanya avunje rekodi ya Ali Daei na lile la ushindi lilipachikwa dk 90+6.

Sasa orodha ya watupiaji katika timu zao za taifa inakuwa inaongozwa na Mreno Ronaldo ambaye ametupia jumla ya mabao 111 anafuatiwa na Daei mwenye mabao 109, 89 ni ya Mokhtar Dahari, 84 ni ya Ferenc Puskas, 79 ni mali ya Godfrey Chitalu,78 ni mali ya Hussein Saeed, 77 Pele na 76 ni Lionel Messi.

Licha ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo Ronaldo alishuhudia penalti yake ikiokolewa na Bazunu mwenye miaka 19 pia hata pigo lake huru liliokolewa na kipa huyo aliyekuwa na siku nzuri kazini lakini alishuhudia timu yake ikipoteza mazima.

Ronaldo amesema kuwa ana furaha moja sio kwa sababu amevunja rekodi ila kwa hali ya kipekee ambayo wanayo hasa kwa kufunga mabao mawili wakati mchezo unakaribia kufika tamati.


"Kukosa penati ni sehemu ya mchezo na ulikuwa ni mchezo mgumu na ushindani mkubwa kila mmoja ameona, ".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic