September 5, 2021


 KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuibukia Arusha leo kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 unaotarajiwa kuanza Septemba 25.

Septemba 25, Simba itakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Baada ya kukamilisha maandalizi ya awali nchini Morocco sasa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inatarajiwa kuweka kambi ya pili Arusha.

Wachezaji ambao wanatarajiwa kuingia kambini ni wale ambao hawajaitwa kikosi cha timu zao za taifa.

Waliopo ni pamoja na Ally Salim, Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu,Jonas Mkude huku Aish Manula, Mohamed Hussein wakiwa ni miongoni mwa wachezaji waliopo timu ya taifa ya Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic