September 8, 2021


 IMEFICHUKA! Kuwa uongozi wa Simba umewaficha mastaa wawili wazawa waliowasajili ambao ni, Kibu Denis na Jeremiah Kisubi ambapo tayari mastaa hao wameanza rasmi programu za mazoezi pamoja na wenzao huku wao wakifanya kwa usiri.


Simba mpaka sasa wamekamilisha usajili na kuwatangaza nyota wapya tisa kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22, huku Kibu aliyetokea Mbeya City na Kisubi aliyekuwa Tanzania Prisons wakiwa bado hawajatangazwa rasmi.

Chanzo chetu cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimelitonya gazeti hili kuwa nyota hao tayari wameanza mazoezi ndani ya Simba tangu siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, licha ya kwamba wamekuwa wakifanya mazoezi hayo kwa siri kwa kuwa bado hawajatangazwa rasmi.


“Tayari Kibu Denis na kipa Jeremiah Kisubi wameanza mazoezi tangu Alhamisi ya wiki iliyopita, licha ya kwamba kwa sasa siyo rahisi kuwaona kwa sababu wamekuwa wakifanya mazoezi hayo kwa usiri mkubwa kwa kuwa bado hawajatangazwa rasmi, hivyo hata picha zao zitatoka tu mpaka kila kitu kiwe sawa,” kilisema chanzo hicho.


Hata hivyo, imeelezwa kuwa kuanzia mastaa hao wameanza mazoezi, wamekuwa wakiwekewa ulinzi mkali sana.


Championi Jumatatu, lilimtafuta Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga kuzungumzia suala hilo ambapo alisema: “Kuhusu suala la Kibu Denis na Jeremiah Kisubi siwezi kuzungumza lolote kwa sasa, Simba haijatoa taarifa zozote juu yao hivyo ni suala la kusubiri ikiwa kuna kitu chochote kuwahusu basi taarifa rasmi itatolewa.”


KIKOSI KIPO ARUSHA

Kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 11 wa Simba Jumapili jioni kiliondoka Dar es Salaam kuelekea jijini Arusha kwa ajili ya awamu ya pili ya kambi yao ya kabla ya msimu ambapo wanatarajia kuwepo huko kwa takriban wiki mbili.


Simba kambi yao ipo eneo la Karatu, sehemu ambayo kuna baridi kali, lakini kukiwa na utulivu wa kutosha na inatarajiwa kucheza huko michezo miwili ya kirafiki.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic