September 8, 2021

 


KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Willian amesema kuwa hakuwa na furaha hata kidogo zama zile alipokuwa ndani ya kikosi hicho.

Raia huyo wa Brazil alivunja mkataba wake wa mshahara mrefu wa pauni 220,000 kwa wiki akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.

Alisepa hapo na kujiunga na Klabu ya Corinthians ya nchini kwao Brazil na alitumika kwenye michezo 37 tu akiwa na timu hiyo na alitupia bao moja tu.

"Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana hakika naweza kusema kuwa sikuwa na furaha nikiwa kwenye timu hiyo.

"Sitaki kuingia ndani sana lakini ieleweke kuwa sikuwa na furaha ndio maana nimeamua kurejea Brazil," .

Nyota huyo alicheza pia timu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic