September 26, 2021

 


BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba wamebainisha kuwa hawakustahili matokeo hayo.

Kwa ujumbe huo ni kama wameyakataa matokeo hayo kwa kuwa walikuwa na nia ya kutwaa tena Ngao ya Jamii ila mambo yalikuwa magumu kwao ndani ya uwanja.

Bao pekee la Yanga lilipachikwa na Fiston Mayele kwa shuti kali lililomshinda Aishi Manula ambaye hakuwa na chaguo dakika ya 10 ya mchezo katika Uwanja wa Mkapa.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba, mabosi hao ambao walikuwa wanaitetea Ngao ya Jamii waliandika kwamba, "Hatukustahili matokeo haya,!"

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na ni kiashiria kwamba Ligi Kuu Bara inakwenda kuanza.

Kesho Septemba 27 ile burudani ya Ligi Kuu Bara inakwenda kuanza na mabingwa watetezi ni Simba.

8 COMMENTS:

  1. Leo hatuoni comments za mashabiki wa timu ya back to back

    ReplyDelete
  2. ,,,wamelala na viatuuuuuuuuuuuu,,,πŸ€ΈπŸ€ΈπŸ€ΈπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

    ReplyDelete
  3. Yanga wastarabu sana, kama simna ndio ingelikua imeshinda saa hiizi mitandaoni pangechafuka kwa matusi mazito mazito. hawa jamaa ni mahayawani sana. Unaona mji ulivyotulia tuli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tangu lini yanga wakawa mastarabu sasa ivi wanaongea sana utafikiri wameingia kwenye makundi CAF champion.Yanga ni wa hapa hapa Tanzania ngoja ligi ianze katkat tu ya ligi utasikia TFF na marefa ni wa Simba.

      Delete
    2. Unaongea makolokolo tu na nonsense mara ligi kuu mara Caf jipeleke mirembe broh

      Delete
    3. HIVI NGAO YA JAMII NDIO KIPIMO CHA UBORA WA YANGA???
      SIMBA NI TIMU KUBWA SANA NA MABINGWA MARA NNE MFULULIZO WA VPL.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic