September 6, 2021


 TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Madagascar. 


Ni Uwanja wa Mkapa majira ya saa 10:00 jioni mchezo huo unatarajiwa kuchezwa.  Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa hakutakuwa na mashabiki kwenye mchezo huo.


Sababu kubwa ya mashabiki kuzuiwa ni suala la kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona hata katika mchezo wa awali uliochezwa dhidi ya DR Congo haukuwa na mashabiki.


Kuhusu mchezo huo Kocha Mkuu wa Taifa Stars,  Kim Poulsen amesema kuwa wapo tayari na watafanya vizuri kwa kuwa wapo nyumbani.

1 COMMENTS:

  1. Plot 89 block 25 makao makuu majengo expo 70 festac 77 sokomoko ushia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic