September 21, 2021


OFISA Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameweka wazi kuwa wanahitaji kufanya vizuri kutokana na maandalizi abayo wameyafanya na wanatarajia kuwa na Usiku wa Ruvu Shooting, Septemba 25, Mlandizi.

Siku hiyo, Ruvu Shooting watafanya matendo ya huruma kwa jamii kabla ya kumaliza na shughuli yao ya Usiku wa Ruvu Shooting.

Bwire ambaye alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Simba kwa sasa bado yupo ndani ya Ruvu Shooting akiendelea kutimiza majukumu yake.

"Tunatarajia kuwa na usiku wa Ruvu Shooting ambapo tutakuwa na wakazi wa Kibaha kufanikisha jambo hili kubwa na muhimu.

"Jambo la msingi ni kuona kwamba kila kitu kinakwenda sawa na kuhusu msimu mpya imani yetu ni kuona kwamba tunaweza kutwaa ubingwa na ikiwa ngumu basi tutamaliza katika nafasi za juu.

"Pia kwa wale ambao wanafikiria kwamba nitakuwa kwenye kashikashi wakipiga hesabu kuniibia simu ama kufanya jambo lolote itakuwa ngumu kwa kuwa kupitia kampuni ya ulinzi ambayo tupo nayo ya Suma JKT  kwa sasa itakuwa ni ngumu kunisumbua pale mechi zinazoitwa kubwakubwa zitakapoisha," . 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic