September 14, 2021

 


KAI Havertz nyota wa Chelsea anaamini kwamba bado Timo Werner ataipa timu hiyo kitu cha tofauti licha ya ujio wa mshambuliaji Romelu Lukaku.

Werner katika msimu wake wa kwanza kikosini hapo alifunga mabao sita ila mambo yalionekana kuwa magumu kwake na alikuwa anakosolewa mara kwa mara.

Havertz amesema:"Lukaku ameleta vitu vingi na ni straika mzuri. Wote tunafahamu kuwa yeye ni mrefu na ana mwili mkubwa. Na sisi kuwa na namba tisa ya aina yake ni kitu kizuri.

"Mfano tuna Timo yeye ni straika ambaye wakati wote anakuwa nyuma na kutafuta mipira. Kwa sasa tuna mastraika wa aina zote,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic