HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanashukuru kwa mapokezi ambayo wameyapata Kagera na ni deni kwa wachezaji hivyo ili kuwalipa ni lazima kupambana kusaka matokeo.
Septemba 27 Yanga iliwasili Kagera ukiwa ni msafara wa wachezaji 25 pamoja na viongozi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Leo Yanga inashuka Uwanja wa Kaitaba kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza.
Manara amesema:"Mashabiki wengi walijitokeza kwa ajili ya mapokezi kwa timu yetu hilo ni deni kwa wachezaji na kulilipa ni muhimu kusaka ushindi uwanjani, mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi bega kwa bega,".
0 COMMENTS:
Post a Comment