October 6, 2021

 



NYOTA wa Simba Henock Inonga Baka leo Oktoba 6 alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiaanaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa.

 Ingizo hilo jipya licha ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu Kombe la Dunia bado amebaki Tanzania akiwa kwenye majukumu ya timu yake.

Sababu inatajwa kuwa ni matatizo binafsi ni jambo ambalo limemfanya nyota huyo ashindwe kujiunga na timu hiyo.

"Jina la Inonga lipo kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya DR Congo ila amekwama kujiunga na timu hiyo kutokana na matatizo binafsi hivyo ataendelea kubaki na timu," ilieleza taarifa hiyo.

Katika mazoezi ambayo yamefanyika leo Oktoba Uwanja wa Boko aliweza kuonyesha uwezo wake katika kutimiza majukumu yake.

Kuhusu wachezaji kuitwa timu ya taifa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa hilo ni jambo nzuri kwa kuwa wanakwenda kutimiza majukumu katika mataifa yao.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic