October 6, 2021


 INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2021/22 David Bryson kwa sasa hali yake inazidi kutengamaa kabla kurejea uwanjani kuonyesha makeke yake.

Bryson aliibuka ndani ya Yanga akitokea Klabu ya KMC yenye maskani yake pale Kinondoni.

Mpaka sasa amekwama kucheza mchezo hata mmoja wa ushindani kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyopata lakini kwa sasa anaendelea vizuri.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga aliweka wazi kwamba wachezaji wake ambao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha ripoti inaeleza kuwa wanaendelea vizuri na wana program maalumu ya kufanya.

Alikosekana kwenye mechi mbili za ligi ambapo Yanga iliweza kushinda kwenye mechi hizo zote.

Ilikuwa Kagera Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Kaitaba na Yanga 1-0 Geita Gold, Uwanja wa Mkapa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic