October 8, 2021

 


KOCHA wa Makipa Yanga, Razack Siwa amefunguka kuwa kinachomzuia kipa wake, Erick Johora kucheza tangu kuanza kwa msimu huu ni ushindani mkubwa anaopata kutoka kwa makipa wenzake ambao ni Djigui Diarra na Ramadhan Kabwili.

 Hivyo kutokukaa kwake benchi kwenye mechi za ushindani na badala yake uwepo wa Kabwili unamaanisha kwamba uwezo wa Kabwili upo juu mazoezini.


Johora tangu asajiliwe Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili hajawahi kucheza mchezo wowote wa ligi pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa pia ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Siwa alisema kuwa: “Nafikiri wote ni makipa wazuri sana kusema ukweli ila nadhani ni changamoto na ushindani mkubwa uliopo ndio maana kila mmoja anataka kupambana ili atimize malengo yake.

 

“Nafasi ya kipa ni moja tu uwanjani tofauti na maeneo mengine kama mabeki, viungo na hata washambuliaji kwa hiyo unapopata nafasi unatakiwa upambane sana na uitendee vema ili anapokuja mwingine aweze kupambana zaidi yako.

 

“Johora hajapata nafasi tu kwenye kikosi ila ni kipa mzuri sana nina imani akipata nafasi anaweza kuonyesha kitu na akapata nafasi kwenye timu kama hao wengine wanavyopata nafasi,“ alisema Siwa.

1 COMMENTS:

  1. Sasa wewe ndugu Kambwili unaona Ni Kipa wa Kawaida? au kwamba alisema ukweli ndiyo maana anabaniwa huyo dogo ,the only Kipa tunaye nchini aliyefunzwa na Ana talent Ni yeye tu .The rest Mpira wa Mchangani tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic