October 4, 2021


 LEO Jumatatu timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia hivyo kwa wale ambao wameitwa ni wakati wa kuanza kujipanga kwa umakini.

Ikumbukwe kwamba ni 2022 michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Qatar ambapo kazi ni kubwa na sio nyepesi kuweza kufika hapo ni lazima mipango iwe makini.

Oktoba 7 sio mbali kwani ipo karibu na mchezo ujao kwa Stars ni dhidi ya Benini hapo Uwanja wa Mkapa kisha kituo kinachofuatwa itakuwa ni Oktoba 10, hapo itakuwa ni marudio nchini Benin.

Kuongoza kundi J kwa sasa haina maana kwamba timu imefanikiwa kufuzu bado kazi inaanza na lolote linaweza kubadilika ikiwa hakutakuwa na mapambano ya kweli.

Hakuna muda mrefu wa maandalizi kwa sasa hilo lipo wazi lakini kupitia muda ambao mtaupata basi wachezaji mnapaswa kutambua kwamba jukumu lenu ni kupambana kwa hali na mali kupata ushindi.

Imani yetu ni kwamba wale ambao wameitwa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen wanatambua kwamba wanakazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Ili kuweza kufanya vizuri ni muhimu kupambana bila kuchoka kwani mechi hizi mbili zitakuwa na picha ya kile ambacho kinahitajika.

Mashabiki jambo ambalo wanahitaji kuona linatokea ni matokeo chanya hivyo kilicho cha msingi kwa muda huuu ni kila mchezaji kuweza kuona anapambana kwa hali na mali.

Ukweli ni kwamba Watanzania wanaimani kubwa na wachezaji hivyo lipeni hiyo imani kwa kutafuta ushindi bila kuchoka. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic