LICHA ya miamba miwili Liverpool na Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kugawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2, Mohamed Salah mshambuliaji wa Liverpool alifunga bonge moja ya bao.
Wakati ubao wa Uwanja wa Anfield ukisoma Liverpool 2-2 Manchester City ni raia wawili wa Afrika waliwatungua mabingwa watetezi ambapo alianza Sadio Mane raia wa Senegal kuwatungua dakika ya 59 kisha Salah raia wa Misri aliwatungua bao moja matata sana dakika ya 76.
Yale ya City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola yalipachikwa na Phil Foden dakika ya 69 na Kelvin De Bruyne dakika ya 81 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lililomfanya Guardiola akatulia kwa kuwa hakuwa na furaha muda wote kwa kuamini kuwa timu yake ilikuwa inaonewa.
Salah alifunga bao hilo bora kwa kupita katikati ya msitu wa mabeki wanne wa City na kuingia na mali ndani ya 18 kisha akachagua eneo gumu kupiga na ngumu kudakwa na kipa kisha likazama mazima nyavuni na katika mchezo huo nyota huyo alikuwa ni staa wa mchezo.
Guardiola amesema kuwa hamna namna matokeo hayawezi kubadilika kwa kuwa kilichotokea kimeshatokea ndani ya uwanja.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa alikasirishwa na namna wachezaji wake walivyocheza hovyo kipindi cha kwanza na hakutarajia matokeo ya aina ile na amefurahishwa na bao la Salah kwa kuwa ni bao bora.
0 COMMENTS:
Post a Comment