October 5, 2021


 CHAMA cha Riadha Tanzania (RT), kwa sasa ki
naendelea vizuri na mazoezi kuelekea mashindano ya riadha ya kitaifa yatakayofanyika Arusha, Oktoba 8 na 9, mwaka huu.

Licha ya kwamba wanaendelea vizuri bado wana tatizo la kukosa udhamini katika mashindano hayo jambo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa RT, Jackson Ndaweka, alisema kuwa wanahitaji kufanya vizuri kwenye hayo mashindano hivyo wadhamani wajitokeze kwa wingi kuwa bega kwa bega nao katika mashindano hayo.

“Mpaka sasa tuna wadhamini wawili tu ambao wameungana na sisi katika michezo ya riadha ambao ni CRDB na Azam TV, hivyo bado wadhamini ni changamoto kubwa kwetu katika kuendeleza riadha na mashindano kwa ujumla.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic