TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imewasili leo Oktoba 11 ikitokea nchini Benin ambapo ilikuwa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Stars jana Oktoba 10 ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin na kukusanya pointi tatu kibindoni.
Ushindi huo imeupata ikiwa ni siku tano zimepita baada ya kulala kwa kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.
Ni bao la Simon Msuva ambaye alipachika bao la ushindi dakika ya 6 na kuifanya Stars kuwa namba moja katika kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin iliyonafasi ya pili.
Msuva ambaye alikuwa na furaha kubwa sawa na wachezaji wengine amesema kuwa ushindi ni zawadi kwa Watanzania.
"Ushindi ambao tumeupata ni zawadi kwa Watanzania kwa kuwa tunapambana kwa ajili ya nchi hivyo ni zawadi kwao nasi tumetimiza majukumu yetu,".
Hongera taifa stars nas tuko nyuma yenu. Mpaka Qatar.
ReplyDeleteHei MPAKA Qatar !!!!!!
DeleteKazi IPO !
Taifa Stars mmenichania mkeka wangu, timu ya hovyo hovyo, mnafungwa nyumbani na kushinda ugenini, hata hivyo hamtofika mbali, Madagascar lazima awafunge si chini ya goli mbili. Kundi hili ni Benin au Madagascar ndio watakao fuzu. Taifa Stars mpira hamna mnacheza mpira wa magazetini.
ReplyDelete