October 11, 2021

 


STAA wa Klabu ya Paris Saint-Germain, (PSG) Lionel Messi ametaja baadhi ya timu ambazo anaamini kwamba zinaweza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu huku timu yake ya zamani ya Barcelona akiiweka kando.

Ikumbukwe kwamba Messi aliibuka ndani ya kikosi cha PSG akitokea Barcelona ambapo alijiunga bure baada ya dili lake kuisha na ilishindikana kuongezewa mkataba mpya kutokana na utaratibu ambao uliwekwa na La Liga katika suala la gharama za usajili.

Alipoulizwa kuhusu timu anayoamini kwamba inaweza kutwaa ubingwa huo Messi aliweka wazi kwamba wengi wanaitaja PSG kuwa inaweza kutwaa ubingwa huo lakini anaamini kwamba zipo nyingine zinaweza kutwaa taji hilo.

Timu ambazo alitaja ni Chelsea,  Manchester United,  Manchester City, Real Madrid, Bayern Munich, Inter Milan huku akiweka wazi kwamba hafahamu kama kuna timu ambayo ameisahau katika orodha hiyo.


"Kuna Chelsea,  Manchester United, Manchester City, Real Madrid ambao kila siku wamekuwa wakifanya vizuri lakini pia kuna Bayern Munich na Inter Milan, sifahamu kama kuna ambayo nimeisahau,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic