October 10, 2021

 


TIMU ya taifa ya Tanzania leo Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90.

Katika mchezo wa leo Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilicheza kwa utulivu mkubwa na kusaka ushindi wa haraka kipindi cha kwanza na baada ya kupata ushindi kazi ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza iliendelea.

Beki wa Stars, Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitumia nguvu nyingi jambo lililopelekea akaonyeshwa kadi ya njano.

Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.

5 COMMENTS:

  1. Hakika vijana wametukonga nyoyo zetu. Asanteni sana vijana wetu mmetetea vema Bendera ya Taifa letu kwenye ardhi ya ugenini tena mbele ya timu iliyotusumbua sana kwa muda mrefu kila tulipo kutana kwenye mechi za mashindano. Na kwakweli Aishi Manula amedhihirisha kuwa yeye ni Tanzania One pasi na shaka

    ReplyDelete
  2. Ila kiukweli kabisa samatta amechoka sana...hakucheza kama captain na hakuwa fit kabisa naomba timu ijiandae kwa maisha bila el capitain

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mchango wake ni mkubwa sana kama umecheza mpira.Kumbuka wanambana maana wanamfahamu,na huo ndiyo muda mzuri wa wengine kufunga magoli

      Delete
  3. Hongera Taifa STARS!
    Hongera watanzania!

    ReplyDelete
  4. Asanteni Sana Taifa Stars kwa kuitetea Tanzania kushinda ugenini. Mioyo yetu imesuuzika. Tunawatakia mafanikio makubwa Sana ktk michezo ijayo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic