MSHAMBULIAJI Marcelin Degnon Koupko raia wa Benin ambaye aliletwa nchini na Yanga kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho, amesepa zake kurejea kwao huku chanzo kikitajwa ni kugoma kujaribiwa mazoezini.
Koupko aliyekuwa akichezea Buffles du Borgou FC ya Benin alikuwepo nchini hapa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita akisubiri kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo arejee nchini kwa ajili ya kuanza mazoezi.
Baada ya kocha Zahera kutua, aliwataka wachezaji wote kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi jijini Dar ili aangalie uwezo wa mchezaji mmoja baada ya mwingine hapo ndipo Mbenin huyo aliposhtuka na kugoma kufanya mazoezi huku akitaka apewe mkataba bila kujaribiwa.
Chanzo kiliongeza kuwa Mbenin huyo alitaka apewe mkataba asaini bila kufanya mazoezi na wenzake akiamini kuwa ana kiwango kikubwa pia anachezea timu ya taifa ya Benin, hivyo hawezi kuanza na majaribio. Baada ya taarifa hizo kocha Zahera aliogopa lawama ya kukubali kumsaini straika huyo kwa kuwa hajauona uwezo wake hivyo mbenini kuuamua kuondoka nchini.
Hiyo ni story ya upande mmoja.Kagere amesainishwa bila ya majaribio.
ReplyDeleteKagere Simba wamemuona lakini huyo Mbenini nani kamuona zaidi ya video clip tu.
DeleteHawawezi leta mtu toka benin wakamtunza wiki mbili...eti hawajui anavyocheza.Tulisikia upande wa Yanga kuhusu Kagere..alipoongea Kagere ni tofauti.
DeleteKweli kabisa, simba wamemuona Kagere akicheza, wala so mchezo 1, mingi tu, hivyo inatosha kabisa, Yanga hawajamuona Hugo Mbenin, namsifu kocha kwakutotaka kuwafurahisha mashabiki wakati kama atakuwa Bomu litamrudia yeye wakati wakubwa wameisha tia pesa mfukoni!kocha ameiona hiyo point!
ReplyDeleteKweli kabisa, simba wamemuona Kagere akicheza, wala so mchezo 1, mingi tu, hivyo inatosha kabisa, Yanga hawajamuona Hugo Mbenin, namsifu kocha kwakutotaka kuwafurahisha mashabiki wakati kama atakuwa Bomu litamrudia yeye wakati wakubwa wameisha tia pesa mfukoni!kocha ameiona hiyo point!
ReplyDeleteHai ndio Abbas Tarimba alikuwa anatusifia kwamba wana scouting??Mchezaji alikuja kwa ahadi ya kusajiliwa na viongozi wa 10%.Amechezea timu ya taifa ya Benin mara ya mwisho dhidi ya Tanzania mwaka jana mechi ya 1-1 huko Benin.Aliingia dakika ya 81.Alishafikia makubaliano ya kusajiliwa nä viongozi.Kocha kataka kumuona jamaa kagoma nä kuondoka.Hawa "mascout"hawakumwona akicheza kabla ya kumtumia ticket?Jamaa sio kichaa ahaidiwe mkataba halafu akute trials.
ReplyDeleteSafi sana.Angejiona yeye ni bora zaidi ya wazawa ilhali huenda uwezo wake ni wa kawaida tu.Tabia hii ya kuwatukuza hawa wageni ndo chanzo cha matatizo yaliyoikumba Yanga na kusababisha wachezaji wazawa wakiongozwa na Kelvi Yondani kuwaondolea uvivu na kuwapa makavu baada ya kuwa wanajikweza
ReplyDeleteNani atalipa gharama za ticket na muda aliokaa Dar?Lazima mtu awajibike.Huu ubabaishaji utakwisha lini
ReplyDeleteKwamba alikataa trials hii ni story ya Yanga..na kwamba alikuja hapa hajulikani si kweli.labda yanga walishindana naye mkataba..tulisikia story tatu tofauti kwa nini Yanga hawakumnasa Kagere..ikiwemo ni mzee, tukasikia wala hatukumtafuta....kumbe walimfuata mpaka holelini akawakataaa.
ReplyDeleteVitu vya ajabu. Nilidhani mchezaji mwenyewe ndiye kakimbia kumbe katimuliwa na Kocha? Mchezaji gani hataki mazoezi? Nani kamleta hapa nchini? Hafai kabisa. Kocha yupo sahihi. SCOUTINGGG TARIMBA UPO WAPI?????
ReplyDeleteAggrey Morris kaongezewa Azam na karibu atakuwa na miaka 34.Watu wanaangalia uwezo.Akija Ronaldo ana miaka 33 mashabiki uchwara wa Tanzania watasema "mzee".
ReplyDeleteHuyu mchezaji kutoa Benin nilimwona kwenye mazoezi hawezi hata kakimbia na kitambi .Scouting my foot upuuzi tu.
Mchezaji atapewaje mkataba bila majaribio? Utatibu wa wapi?
ReplyDeleteNi sawa na kuajiriwa bila kufanya interview.
Ndio maana nchi zilizoendelea hua wanafanya mpaka vipimo ili kuepuka hasara.