October 7, 2021

KING Kibadeni amesema kuwa vijana ambao wanacheza mpira kwa sasa wanapaswa kujituma ili waweze kupata ushindi kwenye mechi ambazo wanazipata tofauti na zamani ambapo hakukuwa na wadhamini wao walikuwa wanacheza mpira na kuondoka.

Kuhusu Simba amesema kuwa ina kikosi kizuri ila watu wanapenda matokea na mechi zake za hivi karibuni haikuwa na matokeo mazuri hivyo inapaswa kutokuwa na haraka. Amesema kuwa wale wachezaji wawili ambao waliuzwa ambao ni Luis Miquissone na Clatous Chama ilikuwa ni biashara hivyo pesa iliyopatikana itatumika kutafuta ushindi. 

Amebainisha kuwa ikiwa Simba watazembea Yanga wanaweza kuchukua ubingwa.

 

4 COMMENTS:

  1. huyo mwandish anajua kwliii tofautiya NMB NA NBC??

    ReplyDelete
  2. Kongole sana Mzee Kibadeni a.k.a Chief Mputa. Kaongea jambo la msingi sana kuhusu umuhimu wa Klabu ya Simba kumpatia tuzo ya kudumu ya kuenzi rekodi yake ya kuwafunga Utopolo FC goli tatu ( hattrick) katika ushindi wa kihistoria wa magoli 6 - 0 walioshinda Simba dhidi ya Yanga mwaka 1977. Anasema, zawadi hii itolewe kila mwaka hadi rekodi yake itakapovunjwa, ina maana hadi atapokuja mchezaji mwengine wa Simba kuifunga Yanga zaidi ya goli tatu katika mechi moja. Naunga mkono hoja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic