October 7, 2021


 BAADA ya kukamilisha dakika 180 za msako wa pointi sita ndani ya Ligi Kuu Bara na kuambulia nne, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamebainisha kuwa ubovu wa viwanja umewanyima uhuru wa kucheza mpira wa pasi nyingi waliouzoea.


Kikosi hicho kilifungua pazia la ligi kwa kucheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Karume, Mara na kushindwa kufungana, kabla ya mchezo wa pili dhidi ya Dodoma Jiji pale Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema: “Ninaweza kusema kwamba ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi, hilo ni jambo zuri, lakini kwetu tulianza kwa tabu kidogo hasa ukizingatia sehemu ya kuchezea haikuwa rafiki kwetu.


“Ukitazama wachezaji wetu wamepambana sana kusaka ushindi ila ilikuwa ni ngumu kucheza ule mchezo ambao tumeuzoea wa pasi pamoja na kuwapa uhuru wachezaji kushinda mapema, hakuna namna lazima mapambano yaendelee," .

Mfungaji wa bao la kwanza kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes alikuwa ni Meddie Kagere alipachika bao hilo Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Alifunga bao hilo akiwa ndani ya 18 kwa shuti la mguu wake wa kulia akitumia pasi ya mshambuliaji mwenzanke, Chris Mugalu.

3 COMMENTS:

  1. Miaka yote viwanja ni hivyo hivyo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila Kuna mabadiliko kwenye mbinu na malengo

      Delete
  2. Misimu yote wanachezeaga vuwanja gani hao makolo fc😂😂😂😂?? Chezeni Mpira,,mlizoea mbeleko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic