October 10, 2021


 VIUNGO wawili wa kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta wanatarajia kusepa ndani ya timu hiyo ifikapo Januari kutokana na kukosa nafasi katika timu hiyo.

Ni Mohamed Elneny na Ainsley Maitland-Niles hawa wawili wanatajwa kwamba wanaweza kusepa ifikapo mwakani 2022, Januari.

Kwa msimu wa 2021/22 mapaka Maitland-Niles ameana katika mechi moja pekee sawa na Elneny ambapo waliweza kucheza kwenye mchezo dhidi ya WestBrom.

Msimu huu utakapomeguka mkataba wa Elneny unameguka na mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote ambayo yameweza kufanyika ila Maitland-Nile yeye mkataba wake unadumu mpaka 2023.

Sababu kubwa ya kuweza kukosa nafasi kikosi cha kwanza ni kutokana na uwepo wa Granit Xhaka, Martin Odegaard, Thomas Partey na Albert Sambi Lokonga. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic