SIMBA SC v Stellenbosch FC ni mchezo wa nusu fainali ya wababe wawili 2024/25 kimataifa wakiwa na rekodi yakumfungashia virago bingwa mtetezi kwenye mashindano ya kimataifa kwa nyakati tofauti.
Aprili 20 2025 mchezo huo
unatarajiwa kuchezwa uwanja wa New Amaan Complex huku Simba SC ya Tanzania
ikiwa na rekodi yakumfangashia virago Zamalek 2003 kwenye Ligi ya Mabingwa
Afrika na Stellenbosch FC wamemfungashia virago Zamalek kwenye Kombe la Shirikisho
Afrika.
NENO LA SEMAJI AHMED ALLY
Ahmed Ally, Meneja wa Idara
ya Habari na Mawasiliano Simba amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye
mchezo huo na wasiwe na presha kwa timu hiyo kutoka Dar na kwenda visiwani.
“Niwaombe watu wa Zanzibar
na hasa mashabiki wa Simba SC wafanye kila kinachowezekana kuipeleka Simba
fainali. Nilisema kila kizazi na historia yake, hii imekuja wakati muafaka na
sisi kuandika historia ya kuipeleka Simba SC fainali. Tufanye kila kinachowezekana Mnyama
kwenda fainali.
“Mpinzani wetu Stellenbosch FC sio timu dhaifu,
hadi inafika hatua hii inaonyesha ni timu ambayo imejiandaa. Wanasimba wote
tulijiandaa kucheza na Zamalek lakini Stellenbosch FC akammaliza pale pale
nyumbani kwake. Hajamtoa Zamalek kwa bahati mbaya.
“Ni kweli ni timu ngeni lakini ina wachezaji
wenye ubora mkubwa na wana kocha mkubwa. Tuna kazi kubwa kwelikweli kuhakikisha
tunamthibiti, tunamfunga ili tukienda kwenye mechi ya ugenini ni iyenaiyena hadi
fainali.
WALIFIKAJE HAPO
Simba SC ilipita hatua ya
nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya penati 4-1 dhidi ya Al Masry baada ya
mchezo wa kwanza ugenini ubao kusoma Al Masry 2-0 Simba, robo fainali ya pili
ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Al Masry hivyo mshindi alipatikana
kwa penati.
Stellenbosch FC wao
walipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Zamalek ambao walikuwa ni mabingwa
watetezi walitolewa kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa nyumbani Aprili 9 2025 baada ya
ile robo fainali ya kwanza ubao kusoma 0-0 kwa timu zote mbili Aprili 2.
KAULI MBIU YA SIMBA SC
Kaulimbiu ya kuingia nusu
ilikuwa HII TUNAVUKA na Simba SC ikafanikiwa, kuelekea fainali Simba SC kaulimbiu
yao inasema HATUISHII HAPA.
Ahmed ameongeza kuwa
malengo makubwa ni kuona kwamba wanatoka katika hatua ya nusu fainali na kufika
hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
SIRI YA SIMBA KUTINGA NUSU
FAINALI
“Kila mtu ni siri yake anajua alifanya nini
Simba kufika nusu fainali. Wachezaji wanajua walipambana vipi Simba SC inafika
nusu fainali, viongozi wanajua walipambana vipi, benchi la ufundi linajua lilitumia
mikakati gani. Rai yangu kila alichofanya mtu kuipeleka nusu fainali kwenye
mechi hii ya kuipeleka fainali basi azidishe mara tatu yake.
“Inawezekana sana Simba SC kucheza fainali
sababu ubora huo tunao na kila kitu kimekaa vizuri. Na bahati nzuri fainali
tutaanzia ugenini na kumalizia nyumbani. Tushindwe nini? Haleluya
Nafasi ya nne Afrika bado
sio malengo ya Simba, nusu fainali bado sio malengo ni sehemu ya mapito.
Tunaitaka nafasi ya kwanza Afrika, sio rahisi kumfikia wa kwanza sababu ya
alama alizonazo lakini tunaanza na kusogea nafasi ya tatu au ya pili lakini
kufikia hilo tunaanza na mchezo wa nusu fainali.
SABABU YA KUHAMA UWANJA
“Kuhama uwanja wapo watu wameanza kuingiwa
ubaridi sababu ya kuhama uwanja, msemo wa Kwa Mkapa Hatoki Mtu umewaingia
Wanasimba, kuhamia Uwanja wa Amaan Simba SC itakuwa na ubora wake uleule. Nipo
hapa kuwatoa hofu Wanasimba kwamba kanzu ndio imebadilika lakini sheikh ni yule
yule.
“Mnyama ni yule yule na
malengo yetu ni yale yale kumfanya vibaya Stellenbosch FC. Asitokee Mwanasimba
kuwa na wasiwasi. Ambacho tungemfanya Stellenbosch katika Uwanja wa Mkapa ndio
tutamfanya Uwanja wa Amaan. Wao waje uwanjani kushangilia mengine watuachie
sisi.
“Ambacho tungemfanya Stellenbosch katika
Uwanja wa Mkapa ndio tutamfanya Uwanja wa Amaan. Wao waje uwanjani kushangilia
mengine watuachie sisi.
“Kama mnavyojua kulitokea
changamoto katika mchezo uliopita hivyo Simba SC tukachagua Uwanja wa Amaan
sababu ni bora lakini pia ni nyumbani pia kwa Simba. Kikosi cha Simba kitawasili
Zanzibar kesho asubuhi, tumeamua kuja mapema ili kujiandaa na wachezaji waanze
kuzoea mazingira ya Zanzibar.
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment