May 28, 2013




Bado inaonekana kuna utata mkubwa kuhusiana na kifo cha msanii wa hip hop, Albert Mangwea ‘Ngwea’.

Ngwea amefariki dunia leo asubuhi katika moja ya vitongoji vya jiji la Johannesburg na baadaye wenzake walimkimbiza katika Hospitali ya St Helen Joseph.

 HII NDIYO HOSPITALI AMBAYO MWILI WA MANGWEA UMEHIFADHIWA..




“Baada ya kufika tuliambiwa ameshakufa, lakini imetushangaza sana,” alisema mmoja wa marafiki zake.

Lakini rafiki yake mwingine ambaye alikuwa mwenyeji wake, alisema Ngwea alikuwa katika hali nzuri tu.

“Alikuwa aondoke leo kurejea nyumbani Tanzania, hivyo niliondoka nyumbani na kumuacha akiwa amelala. Lakini nikiwa njiani nilipigiwa simu kwamba alikuwa hajaamka na walikuwa wanampeleka hospitali.

“Baadaye walinipigia simu kwamba alipoteza maisha tayari. Nilishangazwa sana, hadi sasa sijajua kwa kuwa cheti chenyewe kimeandikwa kizungu lakini unajua mwandiko wa madaktari,” alisema rafiki yake mwingine.

Lakini inaelezwa, Ngwea alirejea nyumbani akiwa anaonekana mchovu na kusema anataka kupumzika.
Siku iliyofuata alichelewa kuamka, hali ambayo iliwashtua wenzake baadaye kabisa.

Hospitali ya St Helen Joseph aliyolazwa iko katika barabara ya 1 Peth, Auckland Park jijini Johannesburg.

Ni moja ya hospitali kubwa lakini inayotibu watu mbalimbali wakiwemo wa kawaida, kwa nyumbani unaweza kuilinganisha na  Muhimbili.

1 COMMENTS:

  1. Mungu Wangu Jamani Tanzania Mbona vijana wanaondoka Taifa Litajengwa na Nani , Kweli ni Kazi ya Mung haina Makosa .Lakini Msiba wa Kijana Unauma Sana Sana.

    Hatuna Jinsi Mungu haiweke Roho yake Mahara Pema Peponi Amina.

    Serikali Tunaomaba Mfanye Mchakato mwili wake urejeshwe Nyumbani Tanzania .

    Ngwea ni Kijana ambaye atakua Mfano wa Kuigwa kwa Taifa Hili La Tanzania mwenye Kipaji Cha Sanaa ya pekee ametumia Kipaji chake kuitangaza Tanzania Ndani na Nje Ya Tanzania hata Huko Mashariki ya Mbali.

    When you Call my Name I will be Their in the King Dom of GOD ..Rest in Peace Jembe Ngwea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic