June 13, 2013



Mabingwa watetezi mara mbili wa michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wametangaza kujiondoa kushiriki michuano hiyo.

Kupitia mtandao wake, Yanga imethibitisha kujitoa katika michuano hiyo ambayo kama wangeshinda wangekuwa wamebeba kombe mara ya tatu mfululizo.

Maana yake baada ya kushinda kombe hilo mara mbili mfululizo, Yanga imeamua kujivua ubingwa.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika nchini Sudan na Yanga imechukua uamuzi huo kutokana na vigezo vya hofu ya kutokuwa na amani ya kutosha nchini humo.

Hofu kubwa ilikuwa ni katika jimbo la Darfur ambalo limekuwa na mapambano ya silaha mara kwa mara.


Kutokana na uamuzi huo, tayari Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limeialika URA ya Uganda kuchukua nafasi hiyo ya Yanga.

Bado URA haijaeleza kama itachukua nafasi hiyo, lakini Shirikisho la Soka Uganda (Fufa) limekiri kupotea barua hiyo.


Timu nyingine ya Tanzania itakayoshiriki michuano hiyo ni Simba nab ado haijajulikana itachukua uamuzi gani kuhusiana na hilo.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic