Kiungo nota wa Arsenal, Mesut Ozil
ameamua kutoa kitita cha pauni 240,000 (Sh milioni 600) alizozipata kwenye
Kombe la Dunia.
Fedha hizo ni Bonus kwake baada ya
kuisaidia timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia kwa kuisunga
Argentina bao 1-0 na Ozil aliahidi hata kabla ya fainali.
Ozil ambaye ki-imani ni Muislam,
amezitoa fedha hizo kusaidia watoto wenye matatizo ingawa haikufafanuliwa
zaidi.
Awali ilielezwa Ozil ambaye ni Mjerumani
mwenye asili ya Uturuki alitoa fedha hizo kwa watu wa Gaza lakini mwakilishi
wake, Rob Harris akafafanua kwamba si kweli kuhusu Gaza badala yake Ozil ametoa
fedha hizo kwenye project za Brazil.
0 COMMENTS:
Post a Comment