Mshambuliaji
mpya wa Yanga, Geilson Santana maarufu kama Jaja atalazimika kuanza kujifunza
Kiswahili kwanza badala ya Kingereza.
Jaja
raia wa Brazil anazungumza lugha moja tu, Kireno na maneno machache ya
kubahatisha ya Kingereza.
Kutokana
na kuzungukwa na wachezaji au Watanzania wengi wanaozungumza lugha ya
Kiswahili, mshambuliaji huyo atalazimika kujifunza maneno ya Kiswahili.
Kikazi
amekuwa hana shida kwa kuwa Kocha Mkuu, Marcio Maximo na msaidizi wake,
Leonaldo Leiva wanazungumza Kireno kama yeye.
Lakini
maneno muhimu kama “nimepita”, “napita”, “nipitishie”, “piga huku”, “achia
mojamoja” ni lazima ajifunze haraka ili kuwasiliana vizuri na wenzake.
Wakati
akiifundisha Taifa Stars, kati ya maneno ya mwanza ambayo alijifunza Maximo
yalikuwa ni “kidogokidogo” na “harakaraka”.
0 COMMENTS:
Post a Comment