Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo kati ya timu ya
Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia
(She-Polopolo) kiingilio cha juu sh.5,000 kwa VIP na sh. 2,000 kwa majukwaa
yaliobakia, mechi hiyo itachezwa ijumaa jioni saa 10 kwenye dimba la Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Twiga
Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage imeendelea kujifua katika hosteli za
TFF zilizopo Karume, kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kuwnaia
kufuzu kwa Michezo ya Afrika nchini Congo- Brazzavile mwezi Septemba mwaka huu.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika wiki tatu zilizopita jijini Lusaka nchini Zambia,
Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Zambia, hivyo
katika mchezo wa ijumaa kuhitaji ushindi wa aina yoyote tu ili kuweza kufuzu
kwa fainali hizo.
TFF
inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa
wingi siku ya ijumaa jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuja kuwapa
sapoti Twiga Stars watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Taifa.
Wakati
huo huo, timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (She-Polopolo) inatarajiwa
kuwasili usiku wa saa 7.25 kuamkia alhmisi kwa shirika la Ndege la Ethiopia
wakiwa na msafara wa wachezaji 18 na viongozi saba na watafikia katika hoteli
ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani Kariakoo.
Msafara
wa Zambia (She-Polopolo) unaongozwa na mkuu wa msafara Lenny Khuwa, kocha mkuu
Albert Kachinga, kocha msaidizi Kape Saili, kocha wa magolikipa Yona Phiri,
daktari wa timu James Nyimbili, mchua misuli Conerlia Chazura, na meneja wa
timu ni Besa Chibwe.
Wachezaji
wanaotarajiwa kuwasili ni Rachel Nachula, Annie Kibanji, Chiko Nkhoma, Osala
Kaleo, Joana Benai, Meya Banda (Nahodha), Misozi CR Chisamu, Jane Nshika
Chalwe, Milika Limwanya, Mary Wilombe, Grace Chanda, Barbra Banda, Memory
Mwaseba, Hazel Natasha Nali, Martha Tembo, Mary Mwakapila na Ireen Lungu.
Kesho
jioni She-Polopolo wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa, uwanja
ambao ndio utakaotumika kw amchezo huo.
Waamuzi
wa mchezo huo kutoka nchini Uganda wanatarajiwa kuwasili leo mchana ambao
ni Ms Anna Akoyi , Ms Nakkito Nkumbi , Ms Jane Mutonyi, na Ms
Nabikko Ssemambo, Kamishina wa mchezo Ms Nomsa Jacobeth Mhalangu kutoka
nchini Afrika Kusini anatarajiwa kuwasili leo jioni.
Mungu ibariki Twiga stars,Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete