July 31, 2016



Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta amezidi kuonyesha makali yake nchini Ubelgiji baada ya kuifungia KRC Genk bao muhimu lililoipa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Oostende.

Karelis ndiye alikuwa wa kwanza kufunga upande wa Genk, ilikuwa ni katika dakika ya 50, Samatta akaongeza katika dakika ya 90+1, yaani katika ile dakika moja ya nyongeza.

Bao hilo la Samatta limekuwa lililoibeba Genk kwa kuwa, Musona aliifungia Oostende bao dakika 90+3 ikiwa ni ya mwisho kabisa baada ya kuongezwa dakika tatu.

Kama ingekuwa bado wanaongoza kwa bao moja la Karelis, maana yake Genk wangeambulia sare ya bao 1-1 baada ya dakika 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic