Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16
mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya
Morocco.
Huku wengi walitegemea ni
nafasi ya kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’, Poulsen amemuita Hussein
Sharrif wa Mtibwa Sugar.
Sharrif maarufu kama
Casillas amekuwa mmoja wa makipa wanaofanya vziuri katika mechi za Mtibwa
Sugar, mfano mzuri ni timu hiyo ilipokutana na Yanga, halafu Simba.
Pamoja na hivyo, kocha huyo amemuita Erasto Nyoni na Aggrey
Morris ambao wamesimamishwa na klabu yao ya Azam FC kwa tuhuma za rushwa.
iye
alikuwa nyota wa mchezo kutokana na uwezo mkubwa.
Mechi hiyo ya mchujo
kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani
nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim,
wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa
kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni
makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula
(Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey
Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani
(Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud ‘Chollo’ (Simba) na Shomari
Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar
(Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank
Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John
Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC),
Mrisho Ngassa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la
ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma
Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk Mwanandi Mwankemwa
(Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela
(Mtunza vifaa).
SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19
Semina elekezi kwa ajili
ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 itafanyika Machi 19 mwaka huu jijini Dar es
Salaam. Washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) siku moja kabla (Machi 18 mwaka huu).
Washiriki hao ni makatibu
wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia
waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari
Tanzania (UMISSETA).
Barua za mwaliko kwa
ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.
0 COMMENTS:
Post a Comment