Kijana mwingine wa Tunisia,
amejimwagia mafuta na kujipiga kiberiti mbele ya hadhira, hali ambayo
imewakumbusha wengi tukio la kijana, Mohamed Bouazizi aliyejiunguza na
kusababisha machafuko Tunisia ambayo yalisababisha kuondolewa kwa Rais Abidine
Ben Ali wa nchi hiyo na baadaye yakatambaa Afrika ya Kaskazini karibu yote,
hasa nchi za Kiarabu.
Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na
miaka 27, hakujulikana jina lake lakini ni maarufu sana kwa mchezo wa soka, na
imeelezwa kwa England amekuwa shabiki namba moja wa Manchester United.
Pamoja na kuipenda Manchester
United, kijana huyo ni shabiki wa Marseille we Ufaransa na anajulikana sana
kutokana na mapenzi yake ya soka.
Kilichosababisha kijana huyo
kuchukua uamuzi mgumu kama huo ni kukosa kazi baada ya kufanya hivyo kwa
kipindi kirefu bila ya mafanikio.
Alikuwa akisumbuka kutafuta kazi
katika eneo la mji wa Jandouba alikokulia, lakini alitoka na kusafiri katika miji
kadhaa bila ya mafanikio.
Mwisho alichukua uamuzi wa kujichoma
moto mbele ya watu, juhudi za kumzima zilifanyika na baadaye akakimbizwa katika
hospitali kwa ajili ya matibabu.
Aliungua sana, haraka hata kwa
kumwangalia inaonekana anahitaji matibabu makini na ya hali ya juu ili kuokoa
maisha yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment