Kiungo wa AEK Athens, Giorgos
Katidis amefungiwa kutokana na kushangilia kwa kutumia saluti ya kinazi.
Katidis alionyesha ishara hiyo ya
jeshi la zamani la Nazi lililokuwa chini ya Fashist Adolf Hitler na leo Shirikisho
la Soka la Ugiriki limetangaza kumfungia maisha kuichezea timu zote za timu ya
taifa.
Kiungo huyo mwenye miaka 20 tayari
amesema hakuwa na nia mbaya huku akilaani vyombo vya habari kulikuza suala
hilo.
Yeye amesisitiza alikuwa
akimuonyesha kidole mchezaji mwenzake, Michalis Pavlis aliyekuwa mbele yake kwa
lengo la kuonyesha furaha yake.
Klabu yake tayari imeeleza inasubiri
maelezo kutoka kwa kiungo huyo ambaye siku hiyo alifunga bao la ushindi kwa
timu yake hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment