*Kutoka
India atupa madongo kwa waliomuondoa madarakani…
PAMOJA na mashabiki 698 kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Simba, Ismail
Aden Rage na kuikabidhi timu kwa Mwenyekiti, Zacharia Hans Pope na Makamu wake,
Rahma Al Kharusi ‘Malkia wa Nyuki’, yeye ameibuka na kupiga.
Rage ambaye yuko katika matibabu nchini India ameibuka na kusema
waliofanya hivyo hawajafanya taratibu huku akiporomosha maneno ya dharau
kwamba, wamefanya mkutano wao uchochoroni huku akiulinganisha sawa na ule wa
harusi.
“Ni mtu mmoja tu anayeweza kuitisha mkutano, ni Ismail Aden Rage na wala
si mtu mwingine. Kwa hiyo Wanasimba watulie nikirudi nitajua cha kufanya,”
alisema ambaye yuko kwenye matibabu nchini India.
“Wangekuwa wanajua wana haki basi wangefanyia mkutano, wameenda
vichochoroni, ndiyo maana nasema mkutano huo ni wa uchochoroni, hakuna kitu
kama hicho,” alisema Rage ambaye anarajia kutua nchini wiki ijayo
Leo mchana wanachama hao, wengi waliokutana ni kutoka katika tawi la
Mpira Pesa ambaow amekuwa na upinzani mkubwa na Rage.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Star Light Cinema jijini Dar es
Salaam, waliamua Hans Pope na Malkia
washike nafasi hizo.
Hata hivyo, tayari Hans Pope
amesema hataweza kuchukua nafasi hiyo na kuwataka wavute subira lakini pia
imeelezwa hata Malkia we Nyuki ametaka kuwe na subira.
Tayari aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ametangaza
kujiuzulu, wiki moja na ushee iliyopita.
Lakini Rage ameonekana ni mgumu kama ‘nyundo’ kujiuzulu huku idadi kubwa
ya wanachama wakiwa wanashauri apumzike.
wanachama hao walifikia uamuzi wa pamoja kuuondoa madarakani uongozi
huo, kutokana na kile kilichoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao na
kuifikisha timu pabaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment