Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la
Shirikisho, Azam FC wamewasili salama salimini nchini Liberia tayari kwa mechi
yao dhidi ya Barrack YC II.
Mmiliki wa wa timu hiyo ni kati ya watu wenye uwezo kifedha
nchini humo, ingawa hata hivyo inaonekana Barrack YC ni kati ya timu change zinazochipukia
kwa kasi.
Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd Maganga amesema kikosi hicho
kimetua salama nchini humo na wanajiandaa na mechi hiyo Jumamosi mjini
Monrovia.
Azam imefanikiwa kuvuka hatua moja baada ya kuitoa kwa aibu
Al Nasiri ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 8-1.
Watoto hao wa Bakhresa walianza na ushindi wa mabao 3-1
nyumbani jijini Dar es Salaam, kabla ya kutoa kipigo kikali cha mabao 5-0
walipokuwa ugenini mjini Juba.
Azam FC inaonekana kuwa na maandalizi ya
kutosha, ingawa inaonekana italazimika kufanya kazi ya ziada kuwashinda
Waliberia hao kwa kuwa ni timu wasiyoijua na si maarufu sana kuweza kupata
taarifa zake za kutosha.
0 COMMENTS:
Post a Comment