Kiatu alichokuwa amevaa beki mkongwe wa Yanga, Stephano
Mwasyika, hivi karibuni kilizua gumzo kubwa kwa mashabiki waliokuwa
wamehudhuria mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es
Salaam.
Mashabiki walianzisha mjadala wakihoji kama kiatu hicho
kilikuwa kikimtosha Mwasyika, ilionekana ni kama oversize.
“Mwasyika anakimbiaje, kile kiatu ni kama kikubwa sana, hebu
angalia jamaa anavyokimbia,” alisema shabiki mmoja na wengine wakaangua
kicheko.
Muda mwingi, waliendelea kumfuatilia Mwasyika, ambaye hata
hivyo alionekana kucheza vizuri ingawa kwa kumuangalia, kiatu hicho kilionekana
ni kikubwa kweli.
Wakati mashabiki hao wanaendelea na mjadala wao huku
wakimfuatilia hatua kwa hatua, Mwasyika alipata pasi nzuri kutoka kwa Said
Bahanuzi, naye aliachia shuti kali lililomshinda Said Mohammed na kujaa wavuni.
Lilikuwa shuti kali lililowashitua wengi waliokuwa uwanjani
hapo na kulazimika kumshangilia.
Shabiki mwingine akasema: “Kumbe kiatu chenyewe kiko fiti
(akimaanisha kinamtosha), kama kingekuwa kinapwaya asingepiga shuti kali kama
hilo.”
Baadaye iligundulikwa kiatu hicho cha Mwasyika ni aina ya
Puma asili yake nchini Ujerumani na si Lotto kama ambavyo baadhi ya mashabiki
walieleza awali.
0 COMMENTS:
Post a Comment