Timu ya
Azam FC iko tayari kwa vita kabla ya kuivaa Barrack Young Controllers siku ya
Jumapili mjini Monrovia.
Lakini uongozi
wa timu hiyo umelazimika kubadili hoteli ukiachana na ile iliyoandaliwa na
wenyeji wake.
Kwa mujibu
wa uongozi wa Azam FC, hoteli hiyo ilikuwa si nzuri ingawa wangeweza kukaa,
lakini kulichowakwaza ni harufu kali ya rangi.
Wameeleza
inaonyesha rangi katika hoteli hiyo ilikuwa imepakwa siku chache zilizopita,
hali iliyofanya kuwe na harufu kali ya rangi na mafuta ya taa.
Kutokana na
hali hiyo, uongozi wa Azam FC ulitaka kubadilishiwa hoteli, lakini Barrack
Young Controllers wakasema wameshalipa kila kitu, hivyo wasingeweza kufanya
mabadiliko yoyote.
Kutokana na
hali hiyo, Azam FC ikachukua uamuzi wa kusonga mbele zaidi na kutafuta hoteli
nyingine.
Azam imefika hatua hiyo baada ya kuing'oa Al Nasiri ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 8-1 katika mechi zilizochezwa Dar es Salaam na Juba.
0 COMMENTS:
Post a Comment