Wababe
wa Uturuki wanaongozwa na Didier Drogba, wamefanikiwa kusonga mbele hadi hatua
ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Galatasaray
iliyolazimishwa sare ya mabao 1-1 nyumbani, wamesonga mbele baada ya kushinda
ugenini dhidi ya Schalke 04 ya Ujerumani kwa mabao 3-2.
Mabao
ya Galatasaray yalifungwa na Altintop katika dakika 37, Yilmaz (dakika 42), Bulut (dakika 90).
Mchezaji
mwingine maarufu Mwafrika anayechezea Emmanuel Ebou aliyewahi kung’ara akiwa na
Arsenal ya England.
Pamoja
na Eboue, mwingine alinyeng’ara katika kikosi hicho jana ni kiungo Wesley
Sneider, Mholanzi ambaye aligoma kutua Man United na kujiunga na Waturuki hao.
Baada
ya sare ya mabao 1-1, wadau wengi waliipa nafasi Schalke 04 ya kusonga hadi
robo fainali. Wajerumani hao walifanya vizuri zaidi katika hatua ya makundi.
KIKOSI
CHA GALATASARAY:
Galatasaray: Muslera, Eboue, Kaya (Zan 78), Nounkeu, Riera, Felipe Melo,
Altintop, Sneijder (Amrabat 70), Inan, Drogba na Burak Yilmaz (Bulut 86).
Subs haikutumika: Iscan, Balta, Kurtulus, Sarioglu.
0 COMMENTS:
Post a Comment