Kama
utabishi basi ni tabia yako, lakini huyu jamaa anaitwa Lionel Messi ni zaidi ya
hatari, alichoifanya AC Milan, hatari sana!
Barcelona
imeonyesha ni timu yenye uwezo mkubwa licha ya kupoteza mechi zake mbili dhidi
ya Real Madrid, pia ya tatu dhidi ya AC Milan, hali iliyosababisha wengi
kuamini imeporomoka kiwango.
Lakini
jana, Barcelona imeitandika AC Milan kwa mabao 4-0 na kufanya iibuke na ushindi
we mabao 4-2, baada ya kuwa imepoteza mechi yake ya kwanza mjini Milan kwa
mabao 2-0.
Baada
ya kupoteza mchezo huo, wengi waliamini Barcelona ilikuwa imetoka katika hatua
hiyo ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora na isingeweza kusonga hadi robo fainali.
Messi
ndiye alikuwa kiwembe baada ya kufunga bao katika dakika ya 5 tu ya mchezo
akionyesha ufundi wa hali ya juu, lakini akipa msumari wa pili katika dakika ya
40.
Waitaliano hao walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao
hayo mawili, kipindi cha pili kiliponza, dakika ya 55, David Villa akapachika
bao la tatu na kuivusha Barcelona.
Lakini ilionekana mapambano yanaendelea na huenda AC Milan
angeweza kutibua mambo.
Huku AC Milan wakiwa wamepanda mbele na kutaka kusawazisha
kwa hali na mali, wakapigwa kaunta atak, beki we kushoto Jordi Alba akamaliza
kazi na kufunga bao la nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment