March 22, 2013



Julio kazini... 
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelo haisi maneno, vichekesho ndiyo usiseme, ana mambo mengi na ukikaa naye hauwezi kusinzia hatya kidogo.

Hivi karibuni ikiwa ni siku moja kabla ya Simba haijaanza safari ya kwenda mjini Bukoba kuivaa Kagera Sugar, Kiwhelo maarufu kama Julio aliamua kueleza namna alivyolipata jina lake hilo la utani la Julio.
Gari la Julio...
 Julio alisema watu wengi wamekuwa wakidhani jina lake hilo ni ujanjaujanja, lakini amepewa na mtu ambaye anaujua mpira vilivyo.
“Mimi bana watu hawajui, hili jina nimepewa na  Alberto Perreira mwenyewe, huyu ni kocha wa zamani wa Brazil kwa wale wanaojua mpira.

“Wakati nikiwa masomoni nchini Brazil, Perreira alikuwa mmoja wa walimu wangu. Sasa tulikuwa tuna kipindi cha kupiga mipira. Tunawekewa magoli halafu yeye anaelekeza upige wapi.


“Sasa mimi kila akielekeza napatia, kila akielekeza napiga palepale, Perreira mwenyewe akasema wewe ni Julio. Ndiko nilikolitoa jina.
“Watu wanadhani nimejitunga tu, mimi Julio napenda vitu tofauti halafu ni mpambanaji. Ndiyo maana unaona hata gari ile pale Mitsubish naendesha mwenyewe tu hapa Dar, kama watu wapo ni wachache sana.

“Napenda vitu vizuri na tofauti, ndiyo maana unaona mambo yangu ni tofauti sana,” anasema Julio huku watu wakiangua vicheko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic