Kocha
Mkuu wa Manchester United, Alex Ferguson amepigwa faini ya pauni 8,500 (zaidi
ya Sh 22.1) kutokana na uamuzi wake wa kugoma kuzungumza na waandishi wa habari
katika mechi ya marudiano dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Old Trafford
jijini Manchester.
Katika mechi
hiyo iliyomalizika kwa Man United kulala kwa mabao 2-1, kilichomuudhi Ferguson
ni kadi nyekundu aliyopewa kiungo wake Luis Nani.
Ferguson
alikuwa akipinga kadi hiyo na mwisho akataka msaidizi wake, Mike Phelan ndiye
akazungumze na waandishi.
Shirikisho
la Soka la Ulaya (Uefa), lilikuwa likifanyia uchunguzi suala hilo na leo
limetoa uamuzi wake na Ferguson amekumbana na adhabu hiyo.
Nani
alipigwa kadi nyekundu baada ya kumrukia beki wa Madrid, Alvaro Arbeloa, lakini
Ferguson akapinga kwamba mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka nchini Uturuki hakuwa
sahihi kuchukua uamuzi huo.
Kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Madrid chini ya Jose Mourinho kiliindoka Man United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa idadi ya mabao 3-2 baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza jijini Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment