England
imeonyesha imepania kupita na kucheza Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani
baada ya kuichapa San Marino kwa mabao 8-0.
England
imeibuka na ushindi huo mkubwa ikiwa ugenini na wenyeji walionyesha tokea
dakika za mwanzo wasingeweza kuuhimili muziki wa England.
England
ilipata mabao yake kupitia Alessandro Della Valle ambaye alijifunga wakati
anajaribu kuokoa katika dakika ya 12. Kinda Oxlade-Chamberlain anayekipiga
Arsenal akaongeza bao katika dakika ya 28.
Wakati
wenyeji wakijiuliza, mshambuliaji mwenye kasi wa Spurs, Defoe akapiga bao
katika dakika ya 36 kabla ya Ashley Young wa Man United kufunga tena katika
dakika ya 39.
Ilionekana
kama England itaenda mapumziko ikiwa na mabao hayo, lakini mkongwe Frank
Lampard akaendelea kuthibitisha kuwa bado wamo baada ya kufunga bao katika
dakika ya 42.
Kipindi cha
pili kilianza kwa England kushambulia mfululizo na Wayne Rooney maarufu kama
Wazza akafunga bao lake katika mechi hiyo katika dakika ya 54, Sturridge akaongeza
katika dakika ya 70 kabla ya Defoe kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 77.
Upande
mwingine, mabingwa Hispania, wakiwa nyumbani walijikuta wakiwa katika wakati
mgumu baada ya kushikiliwa na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na wageni wake Finland.
MSIMAMO ULIVYO..
0 COMMENTS:
Post a Comment