Kumekuwa na
aina mpya ya sanaa, watu wamebuni namna ya kuchora picha za watu maarufu kwa
kutumia visu, sponji na ata vidole.
Lakini safari hii, msanii maarufu kutoka
nchini Polandi, Andrew Lenard amechora picha mbili za wachezaji maarufu zaidi
duniani, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid kwa
kutumia mpira.
Mpolish huyo
ameonekana kwenye mtandao wa akichora picha hizo kwa kutumia mpira ambao
alikuwa akiuchovya kwenye rangi na baadaye kuchora.
Lenard
alisema ameona achore picha za wanasoka hao wawili kwa kuwa ni maarufu na
wanakubalika ulimwenguni kote.
Lakini
hiyo si mara ya kwanza msanii kuchora akitumia mpira, mwaka jana shabiki mmoja
wa mpira wa kikapu, Yi Hong (pichani chini) kutoka jijini Beijing, China alimchora nyota wa
mchezo huo Yao Ming kwa kutumia mpira.
0 COMMENTS:
Post a Comment